TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMATANO MAY 23, 2018.

1.MANCHESTER UNITED ipo tayari kumuuza Winga wake, Anthony Martial kwa pauni €70m.(#TheSun).

2.MSHAMBULIAJI wa PSG, Neymar amewaambia viongozi wa klabu hiyo kuwa anataka kuungana na Jose Mourinho Old Trafford lakini, Mbrazil huyo anaitumia United ili aweze kujiunga na Real Madrid. (#DailyExpress).

3.SWANSEA CITY inamtaka kocha wa Ostersunds FK, Graham Potter. (#DailyMail).

4.LIVERPOOL imeanza mikakati ya kutaka kumsajili Golikipa wa As Roma, Alisson Becker. (#SundayExpress).

5.LIVERPOOL imeanza mazungumzo na FC Barcelona ya kutaka kumsajili Winga wa klabu hiyo, Ousmane Dembele. (#DonBalon).

6.LIVERPOOL & ATLETICO MADRID zinapigana vikumbo kuiwania saini ya Kiungo Mshsmbuliaji wa Juventus, Paulo Dybala. (#Tuttosport).

7.JUVENTUS imeandaa pauni £87.8m za kutaka kumrudisha Turin, Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba. (#Tuttosport).

8.WAKALA Mino Raiola anataka kuwasaidia As Roma katika harakati za kumsajili Winga wa Ajax, Justin Kluivert. (#Calciomercato).

9.ARSENAL inakaribia kumsajili Kinda wa Barcelona mwenye umri wa miaka 15, Joel Lopez. (#Goal).

10.TOTTENHAM HOTSPUR inamuwinda Winga wa Inter Milan, Ivan Perisic. (#FcInterNews).

11.BAYERN MUNICH inamtaka beki wa Hoffenheim, Kevin Vogt. (#Bild).

12.ALVARO MORATA wa Chelsea & DIEGO GODIN wa Atletico Madrid wapo kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa na Juventus. (#GazzettadelloSport).

13.KOCHA wa Juventus, Massimilliano Allegri, anamtaka kiungo wa Lazio, Sergej Milinkovic Savic. (#Tuttosport).

14.LAZIO imethibitisha kuwa Kiungo wake wa Kimataifa wa Serbia, Sergej Milinkovic Savic ana thamani ya pauni €150m.(#IIMessegaro).

15.FC BARCELONA inataka kumsajili beki kiraka wa Manchester United, Daley Blind ambaye yupo kwenye orodha ya wachezaji watakaotimuliwa Old Trafford mwishoni mwa msimu huu. (#DonBalon).

16.TOTTENHAM HOTSPUR & EVERTON zinagombea saini ya Kiungo wa Lille ya Ufaransa, Yves Baruma. (#Le_10_Sport).

17.NAPOLI imethibitisha kuwa beki wake wa kati wa Senegal, Kalidou Koulibaly atajiunga na EPL mwishoni mwa msimu huu huku Chelsea na Arsenal zikiongoza kutaka huduma yake.Msenegal huyo imeelezwa kuwa Ana thamani ya pauni £65m.(#Tuttosport).

18.MSHAMBULIAJI wa Inter Milan, Mauro Icardi anajiandaa kusaini mkataba mpya ndani ya klabu hiyo. Muargentina huyo anatakiwa na vilabu vya Manchester United, Chelsea na Liverpool. Klabu hiyo inadai kuwa Fowadi wake huyo Ana thamani ya pauni €160m.(#Calciomercato).

19.TOTTENHAM HOTSPUR imeungana na Napoli kuiwania saini ya Kiungo wa Fc Barcelona, Andre Gomes ambaye ataondoka Camp Nou mwishoni mwa msimu huu. (#MundoDeportivo).

20.MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann huenda akabaki Wanda Metropolitano baada ya kuwaambia wachezaji wenzake kuwa atabaki klabuni hapo kwa msimu mwengine. (#Marca).

21.WOLVES inawataka nyota wawili wa Marseille, Bouma Sarr na Andre-Frank Zambo Anguissa. (#Telefoot).

22.MSHAMBULIAJI wa PSG, Edinson Cavani anagombaniwa na vilabu vya Chelsea na Ac Milan. (#Lequipe).

23.AC MILAN itajaribu kumsajili Mshambuliaji wa Lazio, Ciro Immobile. (#Tuttosport).

24.MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Robert Lewandowski anataka kuondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu huku Chelsea ikiongoza kutaka huduma yake.