Kocha Unai Emery ambaye amekuwa akitajwa kuifundisha Arsenal, amethibitisha kujiunga na timu hiyo.

Unai ambaye hivi karibuni amemaliza mkataba wake wa kuifundisha PSG, amethibitisha kujiunga na Arsenal kupitia taarifa aliyoiweka kwenye tovuti yake binafsi.

“Proud to be part of the Arsenal family,” ameandika kocha huyo kupitia picha hiyo hapo juu aliyoiweka kwenye tovuti hiyo ikiwa na nembo ya Arsenal.

Hata hivyo Arsenal bado hawajathibitisha taarifa hiyo. Unai ameahi kushinda kombe la Europa League mara tatu mfululizo akiwa na Sevilla na amewahi kufundisha timu nyingine kama Vallencia, Spartak Moscow na nyingine.