Msanii wa filamu nchini Kulwa Kikumba maarufu kama Dude, amefunguka kuwa wanaume ambao wanaanzisha mahusiano nje ya ndoa maarufu kama michepuko wanakuwa na hofu pindi wakirudi nyumbami wakiwa na wake zao.

Dude amesema hayo  kuwa wanaume hao wanakua na wasiwasi mwingi kwa kuhofia michepuko yao, huenda wamenzisha mahusiano na watu wengine kipindi ambacho wanaume hao wapo na wake zao.

“Shida ambayo wanaipata (wanaume) ambao wanachepuka wanakosa ‘control’ kipindi cha usiku kinapofika, wewe unamchepuko basi unalala kwa wasiwasi kwasababu umerudi kwa mkeo, unawaza mchepuko nae anaweza kuwa na mchepuko, mchepuko kachepuka”, amesema Dude.

Dude ameongeza kuwa wasichana ambao wanatenmbea na waume za watu wanatabia ya kuanzisha mahusiano mengine kwasababu hawapendi kuwa na mahusiano na mtu ambaye anamke tayari hivyo wao kutumika kama chombo cha starehe

Muigizaji huyo amewasihi wanaume kuacha tabia ya kuanzisha mahusiano ya nje ya ndoa bali watenge muda mwingi kwaajili ya kuboresha familia zao ili kuepuka migogoro katika ndoa.