Toka Ninyweshwe Madawa ya Kulevya Simuamini Mtu Yoyote- Ester Kiama

MWANAMAMA anayefanya poa kwenye Bongo Muvi, Ester Kiama amefunguka kuwa, tangu akumbane na mkasa mzito wa kuleweshwa madawa ya kulevya amekuwa ni muoga hata kutoka ndani huku akiwa hamuamini mtu yeyote.
Ester aliweka wazi kwamba, maruweruwe ya madawa hayajamuisha vizuri ingawa alishakwenda hospitalini na kupewa matatibu, lakini amekuwa na wasiwasi hata wa kununua chochote dukani kinachohusiana na majimaji.

“Huwezi kuamini kabisa, hata kutoka nyumbani kwangu ninaogopa sana, nimekuwa muoga kupitiliza na sijui hii hali  itaishaje kwa haraka, naona nimepata ugonjwa mwingine wa ajabu sana wa kuwa na wasiwasi,” alisema Ester.

Ester amekuwa katika hali hiyo baada ya juzikati kunyweshwa kinywaji chenye madawa ya kulevya na kuibiwa kila kitu alichokuwa nacho ikiwemo simu mbili na pesa.