Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Simba imetoa wachezaji saba wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa ligi mkuu msimu wa 2017/18.

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF)  imetoa orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo hiyo huku saba wakitokea kwa mabingwa hao wapya wa ligi msimu huu.

Wachezaji hao ni nahodha John Bocco, Emmanuel Okwi, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Aishi Manula, Jonas Mkude na Shiza Kichuya.

Azam wametoa wachezaji watano kwenye kinyang’anyiro hicho ambao ni Yahya Zayd, Razak Abalora, Agrey Morris, Himid Mao na Bruce Kangwa.

Mabingwa wazamani wa ligi hiyo Yanga nao wametoa wachezaji watano ambao ni Kelvin Yondani, Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajibu na Gadiel Michael Michael.

Singida imetoa wachezaji watatu ambao Mudathir Yahya, Tafadzwa Kutinyu na Shafiq Batambuze.

Wengine walioingia kwenye kinyang’anyiro hicho ni Marcel Bonaventure, Adam Salamba, Awesu Awesu, Eliud Ambokile, Shaban Nditi, Hassan Dilunga, Hamis Mcha, Habibu Kiyombo na Mohammed Rashid.

Tuzo hizo zitatolewa Juni 23 Katika ukumbi wa Mlimani City ambapo mbali na mchezaji bora kutakuwa tuzo ya kocha Bora, mchezaji bora kijana, tuzo ya heshima wakati tuzo ya mchezaji kutoka nje ikiondolewa.