Nimefanya Mengi Yasiyo Sahihi Sasa Nimeamua Kutulizana- Shamsa Ford

STAA mwenye mvuto wa kipekee Bongo Movie, Shamsa Ford amesema kuwa, mambo yasiyo sahihi amefanya sana, lakini kwa sasa umefika wakati wa yeye kutulizana hasa kwenye ndoa yake.
Shamsa alisema kuwa, kutokana na kubadilika kitabia anatamani yeye na mume wake wawe mfano imara kabisa kwa jamii yaani waishi muda mrefu sana mpaka Mungu atakapowatenganisha.

“Maisha siku hizi ni mafupi sana, ni muhimu mtu siku ukiondoka uache alama nzuri na ili hilo lifanikiwe ni muhimu kutulizana, jambo ambalo nimeamua kulifanya kwa sasa,” alimaliza Shamsa.