Aunt Ezekiel Awapa Makavu Wanaomsema Kuhusu Kuvaa Nguo Aliyoshonewa na Hamisa Mobetto

MKALI wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefungukia kuhusiana na ishu ya kushonewa nguo na mwanamitindo Hamisa Mobeto, ambayo aliiva siku ya uzinduzi wa filamu yake na kusema kuwa kwa upande wake haoni shida yoyote kwani akivaa nguo aliyoshonewa na mwanamitindo huyo si jambo la ajabu.

Aunt aliliambia Amani kuwa, anawashangaa wanaoshangaa ishu hiyo kwa sababu yeye na Mobeto hawana ugomvi wowote na wala hajawahi kukosana naye, sasa kitakachomfanya ashindwe kuvaa nguo aliyomshonea ni kitu gani?

“Mimi ninawashangaa sana wanaoongea kuhusiana na kuvaa nguo ambayo nimeshonewa na Hamisa. Sioni tatizo kwani tofauti zake na mtu mwingine mimi hazinihusu,” alisema Aunt.

Watu wamekuwa wakimsema Aunt mitandaoni wakihoji kuwa, anakuwaje karibu na Mobeto anayedaiwa kutembea na Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa sasa wakati yeye ni ‘Team’ Zari (Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’, mpenzi wa zamani wa Diamond)!