Dulla Makabila Aikana Tuhuma ya Kubaka Mwanafunzi ''S ijabaka Wala Sina Kesi Polisi"

Msanii maarufu wa singeli Dulla Makabila amefunguka kupitia kuwa hajabaka na hana kesi Polisi kama ambavyo tetesi zinasema.

Msanii huyo amesema kuwa amekuwa akipokea simu nyingi pamoja na familia yake kwa tuhuma ambazo amedai sio kweli na zinapelekea migogoro na mkewe.

“Mambo ya kuzushiwa ni mengi sana hali inayopelekea muda mwingine ugomvi na mke wangu, nimepokea simu nyingi sana kuhusu hilo tukio la kuhusishwa kwenye tuhuma za kubaka lakini mimi nilikuwa mikoani kwenye kazi zangu taarifa hazina ukweli wowote” amesema Makabila

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii kuwa msanii huyo amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kubaka mwanafunzi, mtazame Dulla Makabila akifunguka zaidi hapo chini