Image result for Trump

 Rais wa Marekani Donald Trump ameutupilia mbali mkutano wake wa kihistoria na hasimu wake kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un uoliokuwa umepangwa kufanyika June 12 mwaka huu nchini Singapore.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani ‘White House’, Trump amesema uamuzi wake umetokana na kauli zenye ujumbe unaochukiza kutoka kwa viongozi wa Korea Kaskazini.

Jana Mei 23, 208 Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini, Choe Son-hui alimtukana Makamu wa Rais wa Korea Kaskazini kwa kumuita Mjinga na Mpumbavu kitu ambacho kimezua gumzo katika ulimwengu wa kisiasa na Diplomasia.

Rais wa Marekani, Donald Trump siku ya Jumanne ya wiki hii alisema kuwa Korea Kaskazini ndiyo ingetimiza masharti ya kufanyika kwa mazungumzo hayo.

SHARE
Previous article
Next articleBABU TALE AENDELEA KUSOTA MAHABUSU