Kutoka Ikulu leo May 25 2018 Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Pombe Magufuli amewateua  aliyekua Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Peter Pinda na Makongoro Nyerere kuwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC).

Rais Magufuli amefanya uteuzi huo kwa kutumia mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya CCM toleo mwaka 2017 na majina ya wateule hao yatawasilishwa katika kikao cha NEC kitakachofanyika May 28 2018 Jijini Dar es salaam.