Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Mei 25 ametambulishwa kama mgeni kwa kukaa eneo wanalokaa wageni bungeni hali isiyo ya kawaida.

Haijazoeleka Spika Ndugai kukaa kwa wageni, mara nyingi amekuwa akiongoza Bunge, Ila leo imekuwa tofauti amekaa na mgeni wake, Jaji Mkuu wa Tanzania,Profesa Ibrahim Juma.

Leo Bunge limeongozwa na Mwenyekiti wa Bunge, Azzan Zungu ambaye wakati wa kutambulisha wageni alimtambulisha Spika na mgeni wake,Jaji Mkuu na Spika wabunge ambapo baada ya utambulisho huo walishangiliwa sana na wabunge.