MWANAMUZIKI anayefanya poa Bongo kwenye gemu la Hip Hop, Ibrahim Mandingo ‘Country Boy’, hivi karibuni amefunguka kwamba anasindikiza Mfungo wa Ramadhani, kwa kuzidi kukomaa na muziki wake.

Akichonga na Mikito Nusunusu, Country alisema kwamba yeye si kama wanamuziki wengi ambao mwezi huu husitisha kazi zao, ambapo yeye aliweka wazi kuwa hawezi kuiweka kando kazi kwa sababu Mungu anayemwamini anahitaji watu wafanye kazi ili wapate mkate wao wa kila siku.

“Bila kazi huwezi kupata mkate wako wa kila siku. Hata ukitazama kwenye media mbalimbali duniani hakuna walipositisha kufanya kazi kisa mfungo.

“Mimi pia nitaendelea na kazi zangu, nimeachia Wimbo unaitwa Calabash, nipo na Nikki wa Pili, video yake imefanywa na prodyuza Jozee,” alisema Country