MBUNGE wa Jimbo la Buyungu, wilayani Kakonko Mkoani Kigoma kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kasuku Samson Bilago amefariki dunia leo Jumamosi, Mei 26, 2017 mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati akipatiwa matibabu

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe, ambapo ameeleza kuwa taarifa zaidi juu ya msiba huo zitatolewa muda si mrefu.Bilago pia alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Magharibi na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA.

Bilago alizaliwa Februari 2, 1964 na alikuwa mwanachama wa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Alichaguliwa kuwa mbunge wa Buyungu kuanzia mwaka 2015 hadi mauti yalipomkuta.

Zitto Kabwe kupitia akaunti yake ya facebook amendika;

“Kigoma tumepata pigo lingine. Mwalimu Kasuku Bilago, Mbunge wa Jimbo la Buyungu Wilaya ya Kakonko ametutoka. Amefariki dunia akiwa anapata matibabu hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam.
Ni uchungu usioelezeka kumpoteza Kiongozi Huyu aliyekuwa na mapenzi ya dhati kwa Mkoa wetu, nchi yetu na taaluma ya ualimu. Mungu amlaze mahala pema peponi Ndugu yetu