Muimbaji kutokea WCB, Harmonize amefunguka kuhusu mipango ya kufanya kolabo na msanii Nyashinski kutokea nchini Kenya.

Harmonize amelazimika kulizungumzia hilo mara baada ya kuulizwa na Jembe FM ni kitu gani huwa anazingatia kabla ya kufanya kolabo na msanii mwingine.

“Unajua wimbo wenyewe unakueleza hapa nikimuweka msanii fulani atafaa, let say juzi niliongea na Nyashinski tukapanga tufanye ngoma, akaniambia poa basi mwanagu angalia ngoma unitumie nirekodi,” amesema Harmonize.

“Sasa nikawa najiuliza nimtumie wimbo gani, kila nikiangalia store yangu naona daah, unajua kuna nyimbo nyingine unaona hapa hawezi kukaa kabisa yaani utakuwa unalazimisha. Ila bado nafikiria ni wimbo gani nikampa anaweza akafiti,” amesisitiza.

Utakumbuka Harmonize ameshafanya kolabo na msanii Willy Paul kutokea nchini Kenya ambapo April mwaka huu walitoa wimbo uitwao Pilipili.