Beki wa Real Madrid ambao ni Mabigwa Wapya wa Kombe la UEFA Champions League, Sergio Ramos amesisitiza kuwa hakudhamiria kumuumiza Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah katika mchezo wa fainali uliochezwa jana

Salah alilazimika kutoka katika mchezo huo ikiwa ni baada ya dakika 30 za mchezo kufuatia kuumia bega lake kushoto alipoanguka chini alipokuwa anawania mpira na Ramos

Ramos, ambaye amelaumiwa sana na mashabiki wa soka katika mitandao ya kijamii, kupitia ukurasa wake wa Twitter amemtakia Salah kupona kwema

Aliandika “Muda mwingine mchezo wa mpira wa mguu unakuonyesha upande wake mzuri na muda mwingine upande wake mbaya. Juu ya yote sisi ni ‘professionals’. Upone haraka Mo Salah”

Aidha, Daktari wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Abou El-Ela amesema kutokana na taarifa za madaktari wa Klabu ya Liverpool, Salah ameumia ‘ligament’ hivyo kuna uwezekano akashiriki Kombe la Dunia