Mwanamuziki wa Singeli nchini, Dullah Makabila amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kuwa amekamatwa na jeshi la Polisi baada ya kumtia ujauzito mwanafunzi.
Makabila amesema kuwa habari hizo si za kweli ila kuna watu wasiopenda mafanikio yake ndiyo wanasambaza taarifa mbaya kama hizo wakati siyo kweli na hana skendo kama hilo.
Makabila amesema kuwa taarifa hizo amezipata wakati anarudi kufanya show mkoani Iringa baada ya kupigiwa simu na meneja wa Diamond, Mkubwa Fella kuhusu habari hizo.
Makabila ameendelea kusema kuwa habari hizo zilimshtua sana mpenzi wake pamoja na familia yake lakini walimuelewa baada ya kubaini habari hizo si za kweli.
Habari za mwanamuziki huyo kukamatwa zimeenea kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakifika mbali kwa kusema kuwa tayari Dulla Makabila amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa hilo.
Mwanamuziki huyo kwasasa anatamba na wimbo wake unaoitwa ‘Kuingizwa’ ambao unafanya vizuri katika vituo vya radio nchini.