STAA wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani ametamba kuwa, miongoni mwa majukumu aliyonayo ni pamoja na kumpikia futari mume wake, msanii wa Bongo Flava, Abdul Chende ‘Dogo Janja’.

Irene ambaye ndoa yake ilikuwa na utata mkubwa alisema yeye ni mke wa mtu, tena muislam hivyo anafanya yote lakini anahakikisha anamuandalia futari mumewe.

“Kuhusiana na kufunga, mimi nimezoea kwani siku zote za Ramadhani za nyuma nimekuwa nikifanya hivyo nilipokuwa na Ndiku, sasa hivi nikiwa ni mke halali wa Abdul  natulia nyumbani, napika futari ya mume wangu mwenyewe,” alisema Uwoya.

Ndoa ya Uwoya iliibua utata baada ya baadhi kudai ilikuwa filamu lakini Dogo Janja akakiri ni kweli amemuoa na akasema maisha yanaendelea wote wakiwa ni waislam