BAADA ya Wema Sepetu kutupia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akimpongeza Steve Mengere ‘Nyerere’ kwa kuwa na mtoto mrembo, msanii huyo amejiumauma alipouliza kuhusu anavyojisikia kuwa na mtoto anayefanana naye.

Mtoto huyo ni wa msanii Welu Sengo, binti ambaye aliwahi kugandwa na skendo ya kutoka na Steve na kupewa ‘kibendi’ ila wote kila walipoulizwa walikuwa wagumu kufunguka.

Baada ya picha huyo kuonekana, mwandishi wetu alimpigia simu Steve na kumuuliza kwamba anajisikiaje kuwa na mtoto anayefanana naye, jibu likawa halijanyooka.

“Bwana wewe mimi sijui lolote, waulizwe walimwengu bwana… kama unataka habari andika habari kuwa mimi nitawafuturisha wasanii wote wa Dar es salaam Jumamosi viwanja vya Leaders. Hizi picha siyo mimi niliyezutupia,” alisema Steve na kukata simu.

Lakini baadaye Steve alikiri kuwa mtoto ni wake katika chombo kimoja cha habari na kusema kuhusu mama wa mtoto ‘no comment’.