Baada ya Kimya Kirefu Rudi Aja na 'Niwaze'

MWANADADA kutoka kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ baada ya kukaa kimya kwa muda amekuja na video yake mpya iitwayo ‘Niwaze’.

Ngoma hiyo ameizindua usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Club Next Door jijini Dar es Salaam, ambapo ndani ya wimbo huo ameshirikiana na vijana watatu wa  kundi la The Mafik.

Ruby ameelezea kuwa kolabo hiyo aliyofanya ni baada ya kuwaona vijana hao wapo vizuri katika muziki na akasema video hiyo hakika mashabiki wake wata-enjoy kuitazama kwani maudhui yake yanaendana kabisa na kilichoimbwa.

Video hiyo imeitengenezea nchini Afrika Kusini na tayari inapatikana katika mitandao ya kijamii kuanzia jana ilipozinduliwa.