Leo May 28, 2018 Mwenyekiti wa CCM Tanzania, Rais Dr. John Magufuli ameongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC) katika ukumbi wa Kikwete, Ikulu Dar es Salaam.

Wajumbe Wapya wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa CCM, Waziri mkuu mstaafu, Mizengo Pinda na Makongoro Nyerere wamepokelewa kama wajumbe wapya na kupokelewa kwa shangwe baada ya kukubaliwa na wajumbe wenzao.

Mizengo Pinda na Makongoro Nyerere waliteuliwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa CCM Taifa, John Magufuli.