Ngoma Kupelekwa Afrika Kusini kwa Matibabu

Mshambuliaji mpya wa Azam FC, Donald Ngoma, anatarajiwa kusafiri kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya vipimo vya afya baada ya kukosekana dimbani kwa muda mrefu.

Ngoma ambaye alikuwa Yanga alishindwa kuwa sehemu ya kikosi kutokana na majeraha ambayo yalimshika na kusababisha asicheze takribani msimu mzima unaomalizika leo.

Azam FC walifanikiwa kumalizana na kuweza kuingia naye mkataba wa mwaka mmoja baada ya uongozi wa Yanga kuvunja mkataba wake uliokuwa umesalia.

Mchezaji anatarajiwa kuelekea Afrika Kusini siku yoyote kuanzia leo kufanyiwa vipimo vya afya na baadaye matibabu endapo itabainika inahitajika kufanyiwa hivyo.