Katika Mwezi Huu Hata Mta Mtu Anichokoze Hadi Kunitoboa Jicho Siwezi Kumfanya Lolote- Penny

MTANGAZAJI wa Kipindi cha Harusi Yetu kinachorushwa na Runinga ya Magic Swahili, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amesema kuwa, kwenye mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, hata mtu amchokoze mpaka kutaka kumtoboa jicho lake hatamfanya lolote.
Penny aliiambia Over Ze Weekend kuwa, kwa hivi sasa kila mmoja anatakiwa ajishushe kwa ajili ya kuuheshimu Mwezi wa Ramadhan kwani ndiyo wenye baraka tele.
Penny alisema mwezi huu yuko kwenye maombi mazito na kubwa zaidi analoliomba ni Mwenyezi Mungu amletee mume bora.
“Siko tayari hata kama mtu amenikwaza nigombane naye hata kidogo kwa sababu pia kwenye mwezi huu niko katika maombi mazito ya vitu vingi na kimojawapo ni kumuomba Mungu anipatie mume bora,” alisema Penny.