The Art of Love Ndani ya siku mbili tumepoteza nguvu kazi za Taifa mbili tumempoteza Rose Magombola muuguzi mkuu msaidizi wa hospital ya Mkuranga na Rose Mdenye Muadhiri chuo kikuu cha Dodoma wote kwa kuuwawa na waume zao. Ndani ya wiki hii pia kuna mwanamama kule Lindi kamuua Mume wake kwa sababu ya kumsumbua kupika chakula kingine….. Mwanzoni, wataalamu wa jamii walinzani ukatili wa kijinsia/ Gender based violence (GBV) inawapata wananchi wa vijijini ambao maisha yao ni magumu, walidhani pia inawahusu watu wa tabaka la chini /low class people, pia walidhani inawapata wanawake au wanaume tegemezi, pia walidhani inawapata watu ambao sio wasomi. ….But practices prove them wrong all these hypothesis are not working. Ukatili wa kijinsia ni janga la kidunia halina dini, kabila, rangi, class, kijijini, mjini, mtegemezi, anayejitegemea, msomi, asiyesoma, n.k..The point am trying to insist ni hivi…yaani hawa watu huwa hawauwi mtu kwa siku moja huwa kuna dalili…ukiona mtu kakasirika siku ya kwanza kakupiga, kavunja vitu ndani, mara kamfungia mtoto ndani na kumpiga, mara anafoka mtaa mzima wanawakimbilia, mara unaona ni mtu wa complain kila wakati n.k hizi ni dalili za watu wa aina hii ambao siku moja watakuua, huu ni ukweli mchungu. Cha msingi mtu kuwa makini na mtu uliyenaye katika mahusiano usichukulie poa tabia za ajabu ajabu …kwa Serikali pia huu ni wakati muafaka wa kutenga pesa za kufungua vituo vya therapy Watanzania tupo nyuma sana na Elimu ya Mapenzi Maendeleo ya Taifa huanzia majumbani mwa wananchi wa lile Taifa I mean Bongo sasa tuna ishu nyingi za mauaji kwa chanzo cha Mapenzi HIVI NI MPAKA WAFE WANANCHI WANGAPI NDIO TUTASHITUKA KUWA TUNA TATIZO? ….we have a problem Lets fix it now! – @lemutuz_superbrand

SHARE
Previous article
Next articleSTAA ALIKIBA AMPA SHAVU MPOKI