Msanii mkongwe wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao chake cha ‘Masogange’ Belle 9 amekana tetesi zinazodai kuwa amefulia.

Belle 9 alipata shavu la kusainiwa na label ya ‘Vitamin Music’ ambayo ilimuhamisha kutoka Morogoro na kumleta Dar kwa ajili ya kufanya Muziki lakini baada ya kuoa  Belle 9 alipotea kidogo.

Baadae zilizuka stori kuwa Belle 9 ameamua kurudi nyumbani Morogoro kutokana na kukosa shoo na kufulia hapa Dar kiasi ya kwamba ana kosa hata pesa ya kulipia kodi ya nyumba.

Kwenye Interview aliyofanya na Enews  Belle 9 amekana tetesi hizo za kufulia na kusema hajahama Dar bado yupo mjini:

“Dah Hapana muda mrefu sijafika Morogoro mi Nipo Dar, hizo ni rumors tu zinazosambazwa na watu Lakini pia naona wanasema hivyo kwa sababu sionekani Kwenye maeneo ya starehe mengi.”

Belle 9 amerudi upya na kazi yake mpya aliyotoa siku chache zilizopita inayokwenda kwa jina la ‘Dada’.