Producer Man Walter ameeleza machache iwapo siku moja kutatokea kolabo kati ya Alikiba na Diamond.

Man Walter katika mahojiano na Wasafi TV alipoulizwa kuhusu hilo alisema hajawahi kulisikia ila kama kazi ni kwa ajili ya biashara wanaweza kufanya.

“Mimi sijawahi kusikia kama kuna plan hiyo halafu nimeshaulizwa mara mbili tatu na ninashangaa kwanini swali hilo linakuja kwangu. Hawa ni watu wana management, wana mambo yao, kumbuka mimi nipo jikoni,” amesema.

“Labda kama mtu anataka kuomba msaada kwamba tusaidie kumshawishi mtu, vijana hawa kama wadongo zangu, washikaji zangu na wote nishapiga nao kazi,” ameongeza.

Ameendelea kwa kusema kama ni kazi na ni biashara kwanini watu wasifanye lakini kama kuna vitu vimejificha na vinamaana mbali na kazi ni vigumu.