Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye baada ya Abdularahman Kinana kustaafu kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema kiongozi huyo alibadilisha mtazamo wao kisiasa.

Nape amesema kuwa watamuenzi daima,huku akimtaka apumzike mlezi wao asiye ana mfano.

“Pumzika Rafiki wa kweli, pumzika Mlezi na Mzazi usiyemfano, pumzika Kiongozi, pumzika Komredi. Mwalimu uliyebadili mtazamo wetu juu ya siasa na utumishi kwa umma! TUTAKUENZI DAIMA! Cde. Kinana! Umepanda mbegu na ITAOTA!,” ameandika Nape kupitia ukurasa wake wa Twitter.