Mabingwa wapya wa ligi kuu Tanzania Bara, Simba SC, imefanikiwa kumsajili mchezaji hatari Adam Salamba kutoka Lipuli FC ambaye alitikisa kwenye ligi hiyo iliyomalizika Jumatatu hii.

Simba wamefanikiwa kumsajili Salamba kwa ada ya uhamisho wa shilingi milioni 40 ambapo ataichezea timu hiyo kwa miaka miwili.

Awali mchezaji huyo alizuagumzo wakati Yanga walipomtaka kuichezea timu yao katika mashindano ya CAF lakini maombi hayo yalipigwa chini na timu yake ya Lipuli FC.

Salamba aliifunga Simba kwenye mchezo wa raundi ya pili ya ligi kuu uliochezwa kwenye uwanja wa Samora ambapo bao la kusawazisha la Mnyama lilifungwa dakika za mwisho na Laudit Mavugo na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.