Msanii wa muziki Bongo kutoka kundi la Weusi, G Nako amesema kolabo yake na Vanessa Mdee ‘Wet’ itafika mbali zaidi ya sasa.

Wakati G Nako akipiga stori na JJ wa Jembe FM amesema kuwa wimbo huo toka wakiurekodi walijua utakuja kufika mbali.

“Ni wimbo nzuri toka tulivyoureekodi, wakati albamu bado inaendelea kutengenezwa ilionyesha ni moja ya nyimbo zitakuja kufanya vizuri kwenye albamu,” amesema.

“So nafikiri mafanikio bado yataendelea kuwa makubwa na tunasubiri mafanikio mengine makubwa zaidi na mimi bado nashukuru kwa watu wote ambao wanaendelea ku-support,” amesisitiza.

Wet ni miongoni mwa nyimbo ambazo zimetoka rasmi pamoja na video zake kutoka kwenye albamu ya kwanza ya Vanessa Mdee inayokwenda kwa jina la Money Mondays.