Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameopoa mrembo ambaye ni kiboko wa mzazi mwenzake, Siwema Edson kwa kile kinachosemekana ni mkali balaa, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili.

Chanzo makini kililipenyezea gazeti hili picha za Nay akiwa na mrembo huyo aliyetajwa kwa jina la Martha wakiwa kwenye pozi za kimahaba na kusema kwamba kwa sasa ndiye mchumba wa msanii huyo.

“Hivi mnayo habari? Nay ana chombo kipya ambacho ni kiboko ya Siwema maana ni mrembo balaa ambaye ni mjasiriamali na anatarajia kumuoa, mara nyingi anakuwa naye nyumbani kwake pale Kimara.

“Mimi nakuibia siri ya familia hiyo maana huyo mwanamke ndiye amechukua nafasi ya Siwema hivyo familia imemkalia kooni Nay kwamba lazima aoe mwaka huu lakini amekuwa akisita kufanya maamuzi,” kilidai chanzo hicho. Baada ya kupata habari na picha za wawili hao,

lilimtafuta Nay ambaye aliruka kimanga na kubaki kushangaa imekuwaje picha hizo zikafika kwenye chumba chetu cha habari.

“Sina mpango wa kuoa mimi, umepata wapi hizo picha…sema kwanza picha umezitoa wapi na nani kakutumia ndiyo labda nitakujibu kama ni mpenzi, mchumba wangu au vipi….

“Huyo siyo mwanamke wangu aisee, nina mahusiano yangu mengine kabisa,” aliruka kimanga Nay na baada ya hapo hakujibu tena maswali aliyoulizwa.

Hata hivyo, rafiki wa karibu wa Nay aliyeomba hifadhi ya jina lake alilitonya gazeti hili kuwa, Martha ndiyo kitu kipya cha msanii huyo ila mwenyewe amekuwa akifanya siri.