Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema licha ya vikosi vya ulinzi vya Tanzania kupambana vita alivyovitaja vina sura tatu  vikosi  hivyo viko imara zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali  katika majukumu yake ya kulinda amani.

Waziri mahiga amesema, vikosi hivyo ambavyo vinaiwakilisha nchi vinapolazimika kupigana vinafanya hivyo kama ilivyojidhihirisha kule katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya watu wa Congo.

Dkt. Mahiga amesema hayo katika maadhimisho ya miaka 70 ya kumbukumbu ya walinda amani yaliyofanyika Dar es Salaam na kubainisha kuwa kwa takribani miaka kumi sasa Tanzania imetumikia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa,  miongoni mwao askari 30 waliofariki dunia.

Dkt. Mahiga amesema, Tanzania itaendelea kusimamia utekelezaji wa shughuli za maendeleo za Umoja wa Mataifa ambao unahakikisha Dunia inakuwa mahali salama pa kuishi ili kuweza kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu.