AJALI mbaya imetokea usiku huu wa Jumatatu, Juni 11, 2018 katika maeneo ya Ubungo Riverside jijini Dar es Salaam ambapo gari la wagonjwa (ambulance) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) iliyokuwa ikipeleka mgonjwa katika Kampasi ya Mlimani ikitokea Hosteli za Mabibo, inadaiwa kugongana na lori aina ya scania.

Katika tukio hilo, inadaiwa watu watatu wamepoteza maisha papo hapo ambao ni dereva wa ambulance hiyo, muuguzi (nesi) na dada mjamzito anayedaiwa kuwa ni mwanafunzi wa chuo hicho huku majina yao wote yakiwa bado hayajafahamika mara moja.

Mamlaka husika bado hazijatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo.