Mkubwa Fella Ashtushwa Ishu ya Aslay Kuachana na Mzazi Mwenzie "Nasubiri Nipigiwe Simu na Wahusika Ili Niweze Kusuruhisa"

Mkurugenzi wa kundi la Yamoto Band na Meneja wa Diamond Platnumz, Mkubwa Fella ameshtushwa na taarifa za msanii wa muziki, Aslay kuachana na mzazi mwenzie.

Mkubwa Fella amedai kuwa hakupata taarifa hizo moja kwa moja bali aliziona mtandaoni na kama ni kweli basi anasubiri apigiwe simu na wahusika ili aweze kusuruhisha.

Aslay wiki iliyopita kwenye mahojiano yake na Bongo5 alisema kuwa kwa sasa hayupo tena kwenye mahusiano na mzazi mwenzie akieleza kuwa wameshindwana. Tazama video ya Aslay hapa chini