Amber Lulu Ateswa na Matusi Anayotukanwa Hamisa Mobetto ''Kaza Mwanaume Kama Anakupenda Atarudi"

MSANII wa Bongo Fleva ambaye pia ni muuza nyago ‘video vixen’ Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ amemfungukia mzazi mwenziye na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hamisa Mobeto kuwa, anamsikitikia kipindi anachopitia kutokana na kuendelea kuandamwa kwenye mitandao ya kijamii.
Amber alisema kwamba anaamini Mungu atampigania Mobeto kwa kuwa yanayo-mtokea ni mapito yapo kwa muda tu ikifika wakati kila kitu kitakuwa sawa na furaha yake itarudi kama zamani.

“Mimi namuamini sana Mobeto na ninajua kwamba ni mwanamke anayejiamini kwa kila kitu, kwa hivyo hili lililomtokea ni changamoto tu katika maisha niseme tu kwamba yeye aendelee na biashara zake kwa nguvu zote na kufanya kazi ili aweze kulea familia yake, achukulie hii ndio changamoto ya yeye kukaza buti na kutafuta mkwanja kwa juhudi zote, mwanaume kama anampenda atarudi tu,” alisema Amber.

Hamisa anadaiwa kukumbana na misukosuko kwenye mitandao ya kijamii, baada ya familia ya Diamond kuwa haikubaliani na yeye kuolewa naye licha ya kumzalia mtoto mmoja wa kiume aitwaye Daylan.
chanzo: Global Publishers