Lulu Diva Awapa Makavu Wakina Gigy Money " Mmekimbilia Muziki Ndomana Mmepotea"

MWANA-DADA Lulu Abass ‘Lulu Diva’ ambaye kwa sasa ni miongoni mwa wanamuziki wa kike Bongo wanaotengeneza ‘hit song’ kali, ameibua bifu kwa video queens ‘wauza nyago’ kwamba walikimbilia muziki wa Bongo Fleva na ndiyo maana wamepotea.

Akibonga kiaina na Star Showbiz, Lulu Diva alisema kwamba, anaona kila dalili za wanadada ambao walikimbilia kwenye muziki wakitokea kwenye u-video queen wakipotea wote kwenye gemu jambo linalomfanya kujihisi kubaki bila mpinzani.

“Wote wamepotea, siwezi kuwataja kwa majina nisije kuzua ya kuzua lakini sasa hivi hakuna video queen anayethubutu kubaki kwenye gemu zaidi yangu,” alisema Lulu Diva.

Alipobanwa zaidi amtaje angalau mmojawapo, Lulu Diva alipatwa na kigugumizi. Hata hivyo, video queen wanaojulikana kukimbilia kwenye muziki ni Amber Lulu, Gigy Money, Haitham, Amber Rutty na Agnes Mmasi.
Chanzo: Global Publishers