Nikki Mbishi Awatolea Povu Watangazaji Wanaouliza Kuhusu Alikiba na Daimond
Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Nikki Mbishi ameonyesha kukerwa aina fulani ya uulizaji maswali katika interview.
Nikki Mbishi amesema katika interview maswali kuhusu Diamond na Alikiba ndio hushamiri ila anachojivunia ni kwamba na yeye uhoji pia. Kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika;
Kila interview wanauliza “Una mpango wowote wa kufanya ngoma na Ali Kiba au Diamond?” Hapo basi mtangazaji ndio anajiona kamaliza mwenyewe…#UFALA
Wakiitwa wengine interviews wanahojiwa ila nikiitwa mimi nawahoji wao ndio maana wanakuwa mabubu nikitimba….I’m proud of it. Great monday to all pointless and dumb presenters out there,peace!
September 15, 2017 katika kipindi cha XXL, Clouds FM, msanii Alikiba alikiri kuwa baadhi ya watangazaji wanashindwa kuwa na mtindo mzuri katika kuuliza maswali katika interview.
“Kwanza kabisa unapokuwa unanifanyia interview, mimi nafanya kama mazungumzo ya kawaida na kwa stori ya kawaida mimi nina haki ya kukuuliza chochote ninachojisikia, sio wewe uniulize tu,” alisema Alikiba.