Zimebaki siku tatu Kombe la Dunia la FIFA 2018 linaanza Urusi Alhamisi tarehe 14.

Tayari timu zinaendelea kuwasili Urusi na kuanza kijifahamisha na mazingira

Ujerumani wanawasili kesho Jumatano wakiwa mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia lakini kocha Joachim Low amesisitiza kuwa wachezaji wake lazima waondoe makosa madogo madogo na kila kitu kiwe sawa ili waweze kuhifadhi kombe hilo.

Low anasema wapinzani wamejipanga sawa sawa kwa hiyo vijana wake wanapaswa kuwa makini sana katika kila mechi, lazima wawe macho kuanzia mwanzo na kucheza hadi upeo wao wa juu.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 anasema Kama Ujerumani watakuwa timu ya kwanza tangu Brazil, katika mwaka wa 1958 na 1962, kuchukua mfululizo Kombe la Dunia, basi kila kitu lazima kiwe sawa upande wao