Uongozi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC umefanikiwa kuinyaka saini ya Kocha mkongwe Juma Mwambusi kwa lengo la kuwafundisha wachezaji kwa kipindi cha miaka miwili kutokea sasa.

Hayo yamewekwa wazi na Meneja wa Azam FC, Philip Alando na kusisitiza kwamba lengo la kumchukua Mwambusi ni kutaka kuongeza maboresho katika benchi la ufundi.

“Tumefanya kidogo maboresho kwenye benchi la ufundi kwa kumuongeza mwalimu mzoefu wasiku nyingi ambaye ni mtanzania Juma Mwambusi ambapo kwa sasa atakuwa chini ya kocha Hans na watakuwa pamoja na Idd Nassor Cheche ambaye amekuwa na timu kwa kipindi kirefu”, amesema Alando.

Kocha Mwambusi aliwahi kupata mafanikio makubwa wakati alipokuwa anaifundisha timu ya Mbeya City kwa kushika nafasi ya nne kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara na baadae kutimkia klabu ya Yanga SC kuwa kocha msaidizi.