Kabla Kuja WCB Nilishafanya Kazi na Alikiba- Producer Laiza

Producer kutokea Wasafi Records, Laiza ametaja orodha ya wasanii aliofanya nao kazi kabla ya kujiunga na WCB.

Laiza akipiga stori na Wasafi TV amewataja wasanii hao kuwa Ice Prince, Ommy Dimpoz, Alikiba na Sharo Milionea.

“Kabla ya kuja WCB nilishafanyia kazi ngoma kubwa, za wasanii wakubwa. Nakumbuka nishawahi kufanya kazi na Ice Prince wa Nigeria, nakumbuka nilishawahi kufanya kazi na Ommy Dimpoz, nilishawahi kufanya kazi pia na Alikiba na marehemu Sharo Milionea,” amesema Laiza.

Ndani ya Wasafi Recors, Laiza ametengeneza hits kibao kama Kokoro ya Rich Mavoko, Kwa Ngwaru ya Harmonize, Eneka ya Diamond, Bora Tuachane ya Lava Lava, Kwetu ya Rayvanny, Kijuso ya Queen Darleen, Picha Yake ya Mbosso na nyinginezo kibao.
Chanzo: Bongo5