Baada ya wanachama wa klabu ya Yanga kukutana hapo jana na kuamua kwa sauti moja kukataa barua ya kujiuzulu ya mwenyekiti wao Yussuf Manji hatimaya Mzee Akilimali amefunguka kuhusu nia yake ya kugombea uenyekiti wa klabu hiyo.

Katika mahojiano maalum kati ya Dauda Tv na Mzee Akilimali amesema nia yake ya kuisaidi Yanga iko pale pale na hii ni kutokana na nia yake ya kuisaidia klabu ya Yanga hukua akisisitiza kwamba yuko tayari kama baadhi ya mambo yatafanyika.

Mzee Akilimali amesema kama waziri mwenye zamana ya michezo Harisson Mwakyembe ametoa siku 60 kwa klabu hiyo kufanya uchaguzi haoni sababu ya yeye kutogombea uwenyekiti huo, full video ya mzee akilimali hii hapa tumekuweka Dauda Tv.