Makonda Akabidhi Kadi 220 za Bima ya Afya

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekabidhi kadi 220 za Bima ya Afya (Toto Afya Card) zenye thamani ya zaidi ya shilingi Million 11 kwa watoto yatima na waishio Kwenye mazingira magumu ili wapate uhakika wa matibabu mwaka mzima ikiwa ni sehemu ya Mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Akizungumza  katika hafla fupi ya kukabidhi Kadi  hizo Makonda amesema kuwa kadi hizo zimefadhiliwa na Hospital ya Regency na TMJ za jijini Dar es Salaam na zitakuwa na ndani ya mwaka mmoja kuanzia sasa walipokabidhiwa.
Aidha pamoja na hayo Makonda amesema watoto wengine 400, watapatiwa msaada wa mabegi yenye vifaa vyote  vya shule.
“Kupitia mwezi huu wa ramadhani nawashukuru ndugu zetu wa Regency na TMJ kwa kwa msaada mkubwa wanaoutoa angalau kugusa maisha ya watoto yatima, hivyo leo tumekutana ili kuonesha ishara ya amani upendo pamoja na undugu bila kujali itikadi za vyama na dini” amesema Makonda
Kwaupande wake Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam  Dkt. Daisy Majamba amesema Jumla ya  Card 220 zimekabidhiwa, na kwamba kupatikana kwa watoto hao kulifanyika zoezi la kuwa tambua kutoka katika vituo mbalimbali vya kuelekea watoto jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Hospitali ya Regency Medical Center Dr Rajni Canabar amemshukuru mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Makonda kwa  kuanzisha mchakato wa kumgawa Card hizo na wao kama wadau wamefurahi kushiriki katika kusaidia watoto hao na kuitaka jamii kuwa thamani na kuwa linda watoto hao na kuwa ona sawa na wengine.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi gharama matibabu ya Toto Afya Kadi  ambazo ni kila moja ni shilingi 50400, kwa mwaka ni nafuu ukilinganisha na gharama za matibabu bila kadi  hiyo.
Aidha ameitaka kutambua umuhimu wa Afya kwa Watoto wao kwa kuwa Katia Toto Afya Kard, na kuwataka wadau wengine kujitokeza kuzihuisha kadi hizo baada ya muda wake kwisha.