Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda leo Juni 13, 2018 ameanza rasmi kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, aliyoitoa jana Bakwata Kinondoni kujengwa kwa barabara ya Rashidi Masushi kutoka Bakwata hadi Biafra.

Rais Magufuli alitaka barabara hiyo kupewa jina hilo baada ya mkazi huyo mwenye Jina la Rashid Masushi ambaye ni mjumbe wa nyumba 10 kusema swali lenye maslahi kwa wananchi ambapo alimwomba Rais ukarabati wa eneo hilo lilokuwa likijaa maji mara kwa mara.

Jana,Juni 12, 2018 Rais Magufuli alitembelea kukagua msikiti mkuu wa Baraza Kuu la Waislam(BAKWATA) unaojengwa eneo la Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kutoa agizo hilo.