Rais wa Shirikisho la Spain – Luis Rubiales anaeleza chanzo za kumfukuza Lopetegui: “Tumelazimika kusitisha mkataba wetu na Lopetegui kwa sababu ya tabia yake aliyoionyesha. Amekuwa kocha mzuri kwetu lakini hatuwezi kukubaliana na kitendo alichofanya. Makubaliano yake Madrid yamefanyika bila sisi kufahamishwa, tulikuja kufahamu kuhusiana na hili dakika 5 kabla ya Madrid kutangaza.
:
“Nimezungumza na wachezaji kabla ya kutangaza uamuzi huu na wamenihakikishia kwamba watakuwa na michuano mizuri. :
“Ni kweli baadhi ya wachezaji wakiongozwa na nahodha walinifuata mimi na viongozi wenzangu kujaribu kuzuia uamuzi huu lakini baada ya kufikiria kwa kina, tumefikia maamuzi haya.”