Basi lenye namba za usajili T 755 BAB lililokuwa likisafiri kutoka mkoani Tabora kuelekea mkoani Mbeya, limepata ajali eneo la Igodima jijini Mbeya na kusababisha vifo vya askari kadhaa wa Jeshi la Wananchi. Taarifa kamili tunakuletea.

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinadai kuwa, basi lililokuwa limewabeba wanajeshi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania lililokuwa likitokea Tabora kuelekea Mbeya limepinduka katika mteremko wa Igodima jijini Mbeya.