Dude Afichua Siri ya Kilichomfanya Adumu Miaka Mingi na Mkewe

MKALI wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa, kitu kikubwa kilichomfanya adumu miaka mingi na mkewe Eva ni kutofichana mambo.
, Dude alisema licha ya kupitia ‘mishale’ mingi kwenye uhusiano wake, wamefanikiwa kuikwepa sababu hawafichani mambo.
“Unajua mke wangu amekuwa akisikia mengi sana, mara sijui Ester Kiama, Irene Uwoya sijui nani lakini kwa kuwa nikirudi nyumbani simfichifichi wala sina makandokando, ananiamini kwamba sina mchepuko,” alisema Dude ambaye ana watoto takriban saba, wawili kati yao akiwa amezaa na mkewe anayeishi naye sasa, Eva.