Neema Ndepanya  Awatolea Povu Wanaopenda Kumchamba Wema

MWANADADA Neema Ndepanya ambaye ni meneja wa msanii wa filamu mwenye jina kubwa Bongo, Wema Sepetu, amevunja ukimya juu ya tabia ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipenda ‘kumchamba’ Wema bila sababu za msingi.

Akapiga stori na Risasi Jumatano, Neema alisema kwanza anawashangaa wanaopoteza muda wao kumsema vibaya Wema ikiwa ni pamoja na kumtukana kwani matusi yao hayamfikii.

“Nakereka sana kuona watu wanamchamba Wema bila sababu za msingi, wanapoteza muda wao bure. Kuna wakati huwa nalazimika kuingilia kati pale ambapo wananiingiza na mimi,” alisema Neema.

Mara kadhaa kumekuwa kukiibuka kundi la watu kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram likimshambulia Wema kwa matusi, jambo ambalo limekuwa likiwachefua Team Wema na hata watu wengine waliostaarabika.