Mimi Ndiye Msanii bora wa Kike Hapa Nchini- Odama

MSANII wa filamu Bongo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya J-Film 4 Life, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amejitapa kuwa yeye ndio msanii bora wa kike hapa nchini.
Odama aliyasema hayo hivi karibuni katika mkutano na waandishi wa habari wa kutangaza uzinduzi wa sinema yake mpya ya Mr Kiongozi, uliofanyika katika Hoteli ya Hugo, Kinondoni jijini Dar.
“Unapoiongelea Bongo Movie kwa ujumla, unaniongelea mimi na baadhi ya wasanii wengine, kwa sababu mimi ndio msanii wa kwanza wa kike ambaye nimeanza kutengeneza muvi zangu kwa kampuni yangu,” alisema Odama.
Odama alisema kwenye uzinduzi huo wa filamu yake unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni jijini Tanga, kutakuwa na burudani kabambe kutoka kwa Wasafi Classic Baby ‘WCB’ wakiongozwa na Rayvanny.