Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya vijana wa JKT 11, Askari JWTZ 1 na Dereva vilivyotokea Mbeya.

“Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya ajali ya basi la abiria la kampuni ya Igunga Trans iliyosababisha vifo vya vijana wetu 11 Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), askari 1 waJeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na dereva waliopoteza maisha leo tarehe 14 Juni, 2018 majira ya mchana katika mteremko wa Mwansekwa uliopo Mjini Mbeya”.Rais Dkt.John Pombe Magufuli.