Tanzia: Mume wa Naibu Waziri Angelina Mabula Afariki Dunia

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula.  amepata pigo la kuondokewa na mumewe aliyefariki dunia jana Jumatano, Juni 13, 2018 majira ya saa 11 jioni katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Taarifa ya msiba huo imetolewa leo Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,  na kusomwa na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge,  ambaye amesema marehemu anatarajiwa kuzikwa Mwanza, keshokutwa Jumamosi.
Mwezi Aprili mwaka huu, Angelina Mabula alipata pigo kwa kufiwa na baba yake mzazi, Sylvester Lubala Shimba.