Aliyekuwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Barcelona, Luis Enrique ameteuliwa rasmi kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Hispania.

Enrique amepata nafasi hiyo, baada ya Shirikisho la Soka nchini Hispania kumtimua kocha Fernando Hierro, aliyeshindwa kuiongoza vyema timu hiyo katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.