LEO ni tarehe 11 Julai 2018, zimesalia siku nne tu kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia, ambapo mchezo wa fainali utapigwa Julai 15 mwaka huu.

Kabla ya mchezo wa fainali lazima ipigwe michezo ya hatua ya nusu fainali, ambapo usiku wa jana mchezo wa nusu fainali ya kwanza ulipigwa na ukamalizika kwa timu ya taifa ya Ufaransa kuingia hatua ya fainali, baada ya kuwaondosha timu ya taifa ya Ubelgiji kwa bao 1-0.

Jumatano ya leo utachezwa mchezo wa nusu fainali ya pili. Mshindi wa mechi hii atakwenda kukutana moja kwa moja na Ufaransa, ambaye yeye tayari amekuwa wa kwanza kufuzu hatua ya fainali la Kombe la Dunia mwaka huu.

*Nusu Fainali Ya Pili* :

★Croatia 🇭🇷 Vs 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 England

Muda: 3:00 Usiku

Mwamuzi: Cuneyt Cakir 🇹🇳

Uwanja: Luzhniki.